Free Web Hosting Provider - Web Hosting - E-commerce - High Speed Internet - Free Web Page
Search the Web

Home | Mimi ni Nani | Movie  | Malimwengu | Contact | Michezo | Ngumi | Muziki | Mila | Mavazi | Makala | Guest Book | penpals | Tabia za wasanii | Visa vya wasanii | Maisha ya wasanii | Marafiki | Makala | Realblog | Photoalbum
Ngumi zimeuwa bondia wengi na kuwapatia ulemavu

Bondia wamepoteza viungo na wengine kufa
INGAWA mchezo wa masumbwi unapendwa duniani kote, lakini ni miongoni mwa mchezo unaoleta maafa makubwa kwa wachezaji kama vile ulemavu na hatimaye vifo. hakuna kitu cha kubisha ni ukweli uliomtupu kwamba mchezo huo unaleta madhara makubwa kwa washiriki na jamii ya washariki hao

Mfano hai ni bondia Mohamed Ally jinsi alivyokuwa hivi sasa ni kitu cha kusikitisha, mwili mzima unamtetemeka kutokana na ugonjwa aliokuwa nao wa kiarusi, ugonjwa huo umetokana na makonde mazito aliyokuwa akikabiliana nayo alipokuwa akipanda jukwaani.

Wengi waliomuona mfalme huyo wa masumbwi kwenye ufunguzi wa michezo ya omplick Atlanta Georgia walibubujikwa na machozi, kwa jinsi alivyokuwa akitetemeka.

Madhara ya mchezo huo sio kwamba yamemfika Mohamed Ali tu, bali mabondia wengi wametokewa na athari hiyo kama vile Ulrich Regis aliyefariki baada kupata kipigo kisichokuwa cha kawaida toka kwa Joe Bugnes mjini Shoreditch, katika pambano la raundi 12, bondia Regis alijitahidi kuvumilia raundi zote, mara baada ya kumaliza mchezo alianguka chini na kufariki.

Katikati ya mwaka 1979 mabondia wawili walikufa ndani ya jukwaa baada ya kubondwa na wapinzani wao, miongoni mwao ni mwanamasumbwi wa kutoka Italia, Angelo Jacopucci alikufa baada ya kupigwa na mwingireza Alam Minter. Mwanamasumbwi mwingine aliyeuwawa ulingoni ni Willie Claasen wa kutoka Puerto Rice baada ya kutwangwa na mmarekani, Wilfred Seypion jijini New York, kitu ambacho kiliwastua wapenzi wengi na kuwatilisha hudhuni kubwa.

Hali hiyo iliendelea tena mwaka 1982 wakati bondia wa Afrika Kusini Jacob Morake alipotiwa adabu na mwanasumbwi Brian Mitchell wa huko Afrika Kusini. Morake alikufa saa kumi baada ya pambano kwenye hospital ya Pretoria na kuwafanya ndugu na jama zake kulia kwa uchungu mkubwa huku akilahumu mchezo wa ngumi kwanini umeruhusiwa kuchezwa.

Kama utafwatilia matokeo yanayowatokea wanamasumbwi duniani sidhani kama utapenda kushiriki kucheza kama ukiwa na moyo mwepesi, hasa ukifikilia mateso aliyopata bondia Johnny Owen wa Wales aliyezimia kwa muda wa wiki moja na baadaye kufariki dunia kutokana na kipigo cha bondia Luper Pintor jijini Los Angeler nchini Marekani kwenye mwaka wa 1980 pambano hilo lilikuwa la raundi 12.

Naye Bondia Barry Mc Guigan alimpiga bondia Young Ally wa Nigeria kwa knock out katika raundi ya sita ya mchezo uliofanyika mjini london,Mnigeria huyo alikufa baada ya kufikishwa hospitali na kuwa majonzi kwa wapenzi na washabiki waliomsindikiza kwenye pambano hilo.

Mwaka 1986 Bondia Rocky Kelly wa kutoka nchini uingereza, alimponda bila huruma bondia wa kutoka Scotland Staw Watt kwa knock out na baada ya siku tatu bondia Staw Watt alifariki dunia kutokana na kipigo hicho.Wapenzi wengi hawakukitarajia kifo cha Watt kwa sababu bondia huyo aliondoka ulingoni akiwa ni mtu mwenye nguvu zake huku baadhi ya wapenzi wakimfariji kwa maneno matamu.

Bondia mwingine aliyekufa kutokana na kipigo ni Mmarekani Bradley Stone,alikufa baada ya kubainika kwamba makonde aliyorushiwa yalimualibu ubongo na kusababisha kifo ambacho mpinzani wake Richie Wenton kilimtia hudhuni kubwa.

Richie alisikika akisema kwamba haikuwa nia yake kuuwa bali imetokea kama bahati mbaya kwake, pia hatarajii kitu kama hicho kimtoke siku za mbeleni. Kwani kitu hicho kikikutokea mara kwa mara unakuwa na uwadui na familia za marehemu.

Ukiachana na mabondia waliokumbwa na mikasa ya kufia ulingoni kuna wale waliopata vilema au magonjwa ya akili, moyo na mengine mengine ya kusikitisha mmoja wao ni mwaafrika kusini Daniel Thelele alianguka ulingoni mwaka 1988 baada kupigwa na mwaafrikka mwenzake Aaron Williams, Thelele alipoteza fahamu hapo hapo ulingoni na ndio ukawa mwisho wa mchezo huo.

Naye Mwaafrika Kusini mwingine Brian Baronet, alibondwa makonde mazito na mmarekani Kenny Vice mjini Durban, Afrika Kusini. Makonde ya Kenny yalimfanya Baronent kuanguka chini na kuzimia, alikimbizwa hospital ambako alibaki hivyo hivyo kazimia kwa muda wa siku tatu na hatimaye kufariki dunia.

Mwaka 1989 bondia Rod Doyglas, alisimamishwa katika raundi ya tisa asiendelee kumtwangwa Herol Graham alionyesha dhahari kuwa awezi kuendelea na pambano, laiti kama refa asingetumia uhamuzi huo wa busara nadhani Graham angekuwa maiti.

Baada ya pambano kusimamishwa, madaktari wa walimshauri Graham kwenda hospital kufanyiwa upasuaji wa ubongo kutokana na makonde aliyoyapata ubongo umepata madhara makubwa.

Mwaka 1991 ni miongoni mwa miaka ambapo bondia Michael Watson hatosahau hata siku moja katika maisha yake,mwanamasumbwi huyo alijikuta akipoteza fahamu kwa muda wa wiki 40 (miezi kumi) kutokana na kipigo cha Chris Eu bank wa Wingereza, hivi sasa Watson ni mremavu (amepooza miguu) anatembelea kiti cha magurudumu.

Watson amekuwa mstari wa mbele kushutumu mchezo wa ngumi, nakuomba mchezo huo uwe unachezwa kama vile wanavyocheza ngumi za ridhaa, yaani wawe wanavaa makofia maalumu kichwani ili kudhuiya kichwa kisipate athari kutokana na makonde wanayotupiana wanamasumbwii hao.

Mwaka huo huo bondia Michael Bentt alikimbizwa hospital kuokua maisha yake baada kubondwa barabara na Herbie Hide mjini London.Mara baada ya kupatiwa matibabu na kujiona yuko fiti, bondia Michael Brentt alishauriwa na madaktari kuwa ni lazima hastaafu ndondi bila hivyo anaweza kupoteza maisha yake.

Pambano ambalo wapenzi na washabiki wengine hawatolisahau ni lile la kugombea uzito wa Super Middle lililofanyika mjini Landon februari 25 mwaka 1995 kati bondia Nigel Benn na Gerald Mc Clellan ambalo lilimalizika pande zote mbili za washabiki na wapenzi wakitokwa na machozi.

Vilio vilianza kusikika upande wa mashabiki wa Gerald Mc Clellan ambaye alikuwa amepiga magoti huku akiwa amefumba macho kuashiri maumivu makali aliyoyapata kutoka kwa mpinzani wake.

Tukio hilo la kutisha na kusikitisha liliwafanya wapenzi wake waendelee kupiga mayowe ya udhuni na uchungu, huku wapenzi wa Nigel Benn wakimshangilia kwa nguvu sana, naye Benn akiwa anarukaruka kwa furaha.

Mara Benn alianguka chini na kupoteza fahamu, furaha zote ziliingia kinyongo na watu kuanza kulia kuafuatia hali hiyo. Benn alikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu.

Kwa upande wa Benn uchunguzi uligundua kwamba alikuwa amepatwa na tatizo la kuishiwa nguvu, kwani alitumia (Super Power) nguvu ya mwisho kabisa ya mwanadamu kurushia makonde yake ndio maana akanguka na kuzimia, lakini alitibiwa na baadaye kuruhusiwa na kwenda nyumbani.

Hata baada kutoka hospital Benn alikuwa hapati usingizi kwa mawazo mengi yaliyomtawala kichwani mwake, alisikika akisema, pambano hilo, halikuwa na maana yoyote, ninasikitika sana kumuumiza mwenzangu na mimi mwenyewe kujiumiza naona aibu na kufadhaishwa na hali ilivyokuwa, sijisikii vizuri.

Aliendelea kusema kwamba jinsi pambano lilivyokuwa ninahakika watu wangi walidhani adhabu hiyo ilistahili kuipata mimi na si Mc Clellan. Kwa sababu Mc Clellan alionekana kunidhibiti vilivyo, aliweza kukwepa makonde yangu kwa ufundi wa hali ya juu na kutupa ya kwake yaliyoniingia mwilini sawa sawa.

Bondia mwingine aliyekumbwa na kasheshe ya kubondwa mpaka kufikia hatua ya kuombwa na Daktari wake ni Frank Bruno, ambaye alitakiwa kuacha mchezo wa ndondi na kujishuhulisha na kitu kingine kufwatia maumivu aliyoyapata mjini Las Veges nchini Marekani alipopambana aliyekuwa bingwa wa dunia Mike Tyson, ambaye alipigwa ngumi iliyomchana jicho lake vibaya.

Katika pambano hilo lililouzuliwa na idadi kubwa ya wapenzi na washabiki, Bruno alipigwa kwa knock out kwenye raundi ya tatu na kupoteza ubingwa, kwa mujibu wa maelezo ya daktari wake kama ataendelea kucheza ngumi kuna hatari ya kuwa kipofu mara baada ya kupigwa ngumi ya jicho.

Bondia mwingine aliyekumbana na kasheshe ya kuonja joto la masumbwi katika ulingo ni pamoja na Evendar Holdfied aliyeng'atwa sikio na aliyekuwa bingwa wa mchezo huo Mike Tyson mwaka 1997 katika pambano lililokuwa na kila aina ya upinzani wa hali ya juu hasa baada ya Tyson kupigwa mara ya kwanza na Holdfied.Makala hii imekusanywa kutoka katika vyanzo mbali mbali ya habari duniani.


Lotus
The lotus closes at night and sinks underwater. In the morning it re-emerges and blooms again.
Ngumi zimemsababishia ungonjwa wa kiaharusi kwa Mohamed Ali
Kwa wale waliokuwa wanamfahamu mwanamasumbwi huyo wanaweza kulia.Ikiwa katika nchi zilizoendelea kama Marekani wameanza kugundua kwamba ngumi ni hatari je kama Tanzania ambayo mabondia hawaoni umuhimu wa kupima afya zao, sindio wataweza kujikuta katika matatizo makubwa.

Purple Coneflower
Native American Indians are said to have used this plant for more medicinal purposes than any other plant group.
Andrea Golota alijikuta akipoteza fahamu kutokana na kipigo cha Tyson
Golota alilazimika kutibiwa hospital baada ya kipigo hicho.picha na maelezo zimepatikana toka katika msaada ya web ya Golota na Mohamed Ali