Free Web Hosting Provider - Web Hosting - E-commerce - High Speed Internet - Free Web Page
Search the Web

Home | Mimi ni Nani | Movie  | Malimwengu | Contact | Michezo | Ngumi | Muziki | Mila | Mavazi | Makala | Guest Book | penpals | Tabia za wasanii | Visa vya wasanii | Maisha ya wasanii | Marafiki | Makala | Realblog | Photoalbum
Utafiti wa muziki wa kitanzania
Njenje wafanikiwa kubuni mduara



Hatua walivyofikia wanamuziki wa The Kilimanjaro Band "Wananjenje" ni miongoni mwa mafanikio ambayo wanamuziki wa Tanzania wanatakiwa kuiga kwa ajili ya kufanikisha yale wanayotarajia katika kazi yao ya muziki.

Wanamuziki wa Kilimanjaro Band walikuwa wanajua nini wanachofanya, Kitu gani wanatakiwa kukifanya na kitu gani sio muhimu kwa kukifanya.Ndio maana muziki wao umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kujizolea mamia ya wapenzi na mashabiki katika kila kumbi wanazopiga.

Mafanikio ya bendi yao na muziki wao kwa ujumla yanatokana na kufanya kazi kwa bidii hakuna kitu kingine, Pia wanamuziki hao waliona muziki ni kazi kama zilivyokuwa kazi nyingine ambazo mtu anaweza kuifanya na kujipatia rikizi yake.

Wanamuziki "Wanjenje" kama bendi walikuwa na mikakati yao ya kudumu katika kuboresha ufanisi wa kazi yao, kama vile kutopenda kurekodi mara kwa mara.Kufanya hivyo kunachangia kushusha hadhi ya bendi na ufanisi wa mwanamuziki katika kutunga na hata katika matumizi ya ala.

Jambo hilo wananjenje waliliona mapema na kufahamu hasara yake,ndio maana walipangia mikakati ya kukwepa kurekodi mara kwa mara.

Miongoni mwa hasara ya kurekodi mara kwa mara.Ni pamoja na kuwakimbiza wapenzi na mashabiki kwa ajili ya kuchoshwa na tungo za mara kwa mara za bendi husika.

Kitu kingine ambacho kinawasaidia Wananjenje mpaka kufikia muziki wao kuwa wa hali ya juu ni pamoja na kuto kubali kupiga kwa kiingilio soda ama bia kama ilivyokuwa kwa bendi nyingine za Tanzania.

Njenje iliyoanzishwa katikati ya mwaka 1973 mpaka muda huu wamerekodi santuri tatu, lakini utashangaa kuona kuna bendi zimeanzishwa katikati ya mwaka 1980 mpaka 2002 zimekwisha rekodi zaidi ya santuri tatu.

Kati ya santuri hizo hakuna hata mmoja iliyovuma ama kujipatia umaarufu kama ilivyokuwa kwa santuri za Wanjenje,pia hakuna santuri iliyokuwa na ubora wa sauti kama ilivyokuwa kwa santuri zilizotengenezwa na bendi ya Kilimanjaro "wananjenje"