 |
| |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
 |
| Umuhimu wa mavazi na namna ya kuvaa........... |
 |
|
Kuna mavazi ya kazini na kutokea katika matembezi
Hivi sasa utaona wasichana waliokuwa wengi wanavaa nguo za ajabu na kwenda nazo kazini,wengi wa wasichana wa siku hizi ni malimbukeni wa hali ya juu kutokana na kushindwa kuchagua nguo za kuvaa.
Katika mahojiano yaliyofanywa na mwandishi wa makala haya na mfanyakazi mmoja wa duka la nguo la jijini aliyejitambulisha kwa jina la Badula Al Haji amesema wasichana wengi hawajui nguo gani ya kazini na nguo gani ya kutokea.
Kutokana na kutokuja wamekuwa wakivaa nguo za kwendea katika maonyesho mbali mbali ya usiku na kuvaa mchana kwa ajili ya kwendea kazini.
Inakuwa sio vizuri msichana kuvaa kimini na kwenda nacho kazini ama kanisani kama wanavyofanya baadhi ya wasichana, hali hiyo inachangia kumuonyesha namna gani hiyo msichana alivyokuwa mshamba.
|
|
|
Kuvaa koti ama suti wakati wa jua ni ushamba Utakuta baadhi ya wanaume washamba licha ya wenyewe kujifanya wajanja, wanavaa suti ama koti wakati wa jua kali na kutembea kwa miguu huku wakijifuta majasho.
Wengi wanashindwa kufahamu kuwa mavazi sio kitu kinachoweza kumfanya mtu kuaminika mbele ya watu.Kama unakipaji hicho hata uvae suti na koti bado utaonekana ni mbabaishaji.
Katika jiji kama Dar es Salaam ambalo joto ni nyumbani kwao, utamkuta mtu amefunga tai na koti huku akitembea kwa miguu na kutokwa na jasho kiasi cha kutaka kujaza ndoo ya maji.
Ushamba au washamba wapo wengi katika mambo ya uvaaji na hata matendo yao, mara nyingi watu wanaopenda kuvaa tai na makoti wanatabia ya kunyenyekea mabosi.
Akitoka hapo naye anataka kunyenyekewa kwa sababu amevaa sawa na bosi wake anayetembea na gari hata akivaa koti hawezi kupata majasho kama yeye anayekwenda na miguu kutwa mzima na baadaye kupanda daladala lilikuwa limejaa watu wengi huku harufu za ajabu zikiwa zinatoka kwa watu mbali mbali waliovaa makoti na kuwa kichefuchefu kwa wale wasiovaa makoti.
|
|
Unatakiwa kuvaa kulingana na mwili wako
Kuna baadhi ya watu wengi hasa wasichana wanaweza kuvaa nguo yoyote ili mradi amemuona mwenzake amevaa na kupendeza, lakini ameshindwa kufahamu mwenzake amevaa hivyo kutokana na mwili wake ulivyo.
Utakuta msichana amemuiga mwenzake kuvaa kimi wakati miguu yake ni mwembamba kama mikono ya miwani.Ukitaka kuvaa kimi lazima uwe na mguu wa nguvu wa chupa ya bia na sio wa mikono ya miwani.
Ni ushamba na ujinga mkubwa kuvaa nguo ya kubana wakati huna matako makubwa, nguo ya kubana inampendeza zaidi mwanamke mwenye matako makubwa.
Uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa mavazi wamesema kwamba mwanamke mnene kiasi ndiye anayependa zaidi kwa mavazi ya kubana.
Pia wamesema kwamba wanawake wanene wanamvuto mkubwa katika mapenzi tofauti na wanawake wembamba"Ma miss", lakini kutokana na kwamba wanawake wanene ni wazito katika kufanya maamuzi ndio maana wakapendekezwa wanawake wembamba kushiriki katika matangazo mbali mbali na hata katika mashindano ya urembo.
|
|
|