|
Wachezaji,Mabondia kukabiliwa na kichaa
DAKTARI wa mchezo wa ngumi za kulipwa. Mecky Matee alisema mabondia wanahatari kubwa ya kupatwa na magonjwa ya kichaa kutokana na ngumi wanazokabiliana nazo wanapokuwa ulingoni.
Matee alisema mabondia wengi wanarushiana ngumi za kichwani, ambazo zinaweza kuleta madhara kwenye ubongo na kusababisha matatizo ya akili.
Akizungumza katika semina ya makocha,waamuzi na mabondia, Matee alisema ndio maana mabondia wa ngumi za ridhaa wanavaa kofia za kuzuiya ngumi.
Hata hivyo Matee alisema kofia hizo hazizui maumivu ya ngumi bali inaweza kupunguza kwa kiasi fulani, ukilinganisha madhara atakayopata mtu aliyevaa kofia na asiyevaa ni tofauti.
Alisema ndio maana mabondia wanashauri kupimwa afya zao mara kwa mara ili kuweza kuwa na uhakika wa afya yao.
Matee alisema mchezo wa ngumi ni mchezo hatari sana kwani unaweza kupoteza maisha ya bondia, au kumfanya bondia kuchanganyikiwa na kushindwa kufanya yale aliyokuwa akifanya kabla ya kuchanganyikiwa.
Alisema madhara ya mchezo wa ngumi yanaoneka baada ya muda mrefu, mhusika anaweza kupoteza kumbukumbu na kuanza kuzungumza vitu ambavyo havifahamiki.Pia anakuwa mkali sana tofauti na alivyokuwa mwanzo kabla ya kuanza kuchanganyikiwa.
Kauli alizotoa daktari huyo zilidhibitishwa na aliyekuwa bondia wa ngumi za ridhaa Tanzania. Emmanuel Kimaro ambaye kwa sasa anafanya kazi ya kutuliza vurugu katika baa ya Man hunter.
Kwa mujibu wa maelezo yake Kimaro alisema ngumi zimemsaidia sana kuweza kujenga nyumba wake kijijini kwao moshi, pia amefanikiwa kununua mifugo kama vile ng'ombe na mbuzi.
Alisema licha kuweza kumiliki vitu kama hivyo, lakini anakubali kwamba ngumi zimemchanganya akili zake, alisema kuna wakati anakuwa na akili timamu na kufaikiria mambo mbali mbali ya maendeleo kwa ajili ya familia yake.
Kimaro alisema kuna wakati anajikuta anafanya vitu vya ajabu hata akimbiwa baada ya akili zake kutulia anakuwa hakubali kama alifanya vituko hivyo.
Alisema ngumi ni mchezo mzuri sana, lakini madhara yake ni makubwa. Alisema bondia yoyote anapokuwa ulingoni anakumbana na ngumi nzito za kichwa toka kwa mpinzani wake.Alisema ngumi hizo zinasababisha matatizo makubwa kwa bondia. Matatizo hayo yanaonekana baada ya muda mrefu kupita.
Kimaro alisema mbali ya yeye kuwa na matatizo hayo, alisema kuna mabondia wengine ambao ni watu wa makamo hivi sasa wanasumbuliwa na matatizo kama yake.
Alisema sio vizuri kuwataja lakini mabondia waliacha mchezo wa ngumi muda mrefu lakini matokeo ya mchezo huo yanaanza kuonekana hivi sasa.
Kimaro alisema kwa vile mchezo huo ni wahatari mabondia wanashauri kucheza kwa vipindi maalamu, kwa ajili ya kuweza kulinda afya zao.
Alisema kutokana na shida walizokuwa nazo mabondia wa tanzania wanajikuta wakichezwa kila mara kwa malipo madogo, alisema hali hiyo inachangiwa na mapromota wanayejali fedha na kuliko afya ya binadamu.Wanawachezesha mabondia huo mara kwa mara na hatimaye kuwafanya kuwa wagonjwa.
"Kama unaona utani anza kuwachunguza mabondia wote unaowafahamu utagundua kuwa akili zao sio timamu, mimi najijua akili zangu sio timamu, lakini kuna mabondia ambao wanajiona kuwa ni fresh wakati si kweli",alisema Kimaro.
Alisema hata kwa mabondia wa nje ya Tanzania wengi wanamataizo ya akili, alitoa mfano wa bondia Mike Tyson jinsi anavyofanya mambo ya ajabu, Prince Nassem wa Uingereza naye anafanya mambo ya ajabu.Alitaja mabondia kama Sugar Ray, Chriss Ubank na wengine.
Taarifa za kupata matatizo kwa mabondia zinaonekana ndio muhimu sana,lakini wanashindwa kuelewa kuwa hata wachezaji wanaweza kupata matatizo ya akili kutokana kupiga mipira ya vichwa.
Lakini jambo ambalo pengine wachezaji wa mpira hawalijui ni kwamba, kwa kutumia kichwa chake kupiga mipira tena na tena anaongeza uwezekano wa yeye kupata madhara ya kudumu na hitilafu fulani katika ubongo wake.
Kulingana na taarifa za utafiti kwa wachezaji wa kulipwa ambao pengine hucheza kandanda mara moja kwa wiki, bado wanahatarisha maisha yao; kupuuza dalili za maumivu kama, kuumwa kichwa, kusikia kizunguzungu, kupoteza kumbukumbu na kupoteza umakini katika kazi za kutumia akili, huongeza hatari zaidi kwa maisha ya mchezaji.
Kufuatana na wataalamu wa tiba, akiwemo mtaalamu maarufu wa tiba wa Afrika Kusini, Profesa Tim Noakes wa Taasisi ya Sayansi-Michezo ya Cape Town, wanasema kuna mashaka kwamba watu wanaopata makonde, kipigo na kugonga mipira kwa kichwa, baada ya miaka kadhaa inayofuata kuna uwezekano wa kupata madhara fulani katika ubongo wao.
"Kuna uhusiano wa wazi kabisa, kitu chochote kiletacho madhara kikirudiwarudiwa katika sehemu moja ya mwili, huhatarisha maisha ya mtu huyo" anasema Profesa Ann Jordan wa Idara ya Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Rhodes, mjini Grahamstown.
Profesa Jordan ameshawafanyia majaribio wachezaji wa rugby wa Chuo Kikuu cha Rhodes na amegudua kuwa kuna dalili za wazi kabisa zinazoonyesha kuwako uharibifu katika ubongo, hususan kwa wachezaji wa mbele ambako kuna migongano mingi ya vichwa.
"Si lazima iwe migongano ya nguvu sana kichwani, kila mgongano unaleta madhara kwa kiwango chake, ambapo baada ya mapumziko ya kutosha madhara hayo hupona yenyewe. Lakini kama ubongo utatikiswa tena kabla ya mapumziko ya kutosha, basi madhara yanaweza kuwa makubwa sana na yasiyoponyeka tena" anasema Mtaalamu wa Ubongo wa Norway.
" Na kama unapata migongano mara kwa mara kichwani, uwezekano wa kupata madhara katika ubongo ni kati ya asilimia 80 na 100" anaongeza kusema.
Ulimwengu unafahamu madhara ya afya za wanamasumbwi kwa muda mrefu sasa. Lakini taarifa za utafiti za hivi karibuni kuhusu wanakandanda kuishia katika taasisi za tiba za matatizo ya ubongo zimeutikisa ulimwengu wa kandanda kwa mshangao.
Kufuatana mtaalamu huyo wa Norway, anasema kuwa kupiga mipira kwa kichwa mara kwa mara husababisha madhara sawa na yale ya kupigwa makonde mazito kichwani kwa wanamasumbwi.
Wachezaji mpira hukabiliana na uwezekano mkubwa wa tatizo hili katika ubongo wao hasa katika umri wao mdogo, hususan kupoza kumbukumbu, kutokuwa makini, matatizo katika misuli na kubadilika tabia.
"Mchezaji kijana anayepuuzia dalili kama vile; kizunguzungu, kuumwa kichwa na kuchanganyikiwa anaweza kupata matatizo makubwa katika kujifunza na hatimaye kupata dalili za kichaa" anaongeza mtaalamu huyo.
Wamelinganisha vipimo vya aina ya "hi-tech scans" kwa ubongo wa wachezaji 15 wa kandanda,17 wa mpira wa miguu wa Wamarekani "American football" na wanaume 20 wasiocheza mchezo wowote, wote waliofanyiwa majaribio ni wenye umri kati ya miaka 20 na 30".
Wachezaji wote waliofanyiwa uchunguzi huo, walidhihirika kupata migongano mikubwa katika vichwa vyao ambapo wachezaji 11 walipatikana na majeraha kadhaa kwenye ubongo.
Ingawa mchezo wa "American football" ni wa maguvu sana na unaoonekana wenye hatari kuliko mpira wa miguu, ni wachezaji watatu tu waliopatikana na madhara kadhaa kwenye ubongo wao, sababu ni kutokana na wachezaji wa mchezo huo kuvaa kofia mgumu kichwani "helmet".
Daktari Ed van Wijk, Mwenyekiti wa chombo cha ndondi nchini Uholanzi, anaelezea tukio moja wakati wa michezo ya kombe la dunia nchini Ufaransa ambapo mchezaji wa Uholanzi alijigonga kichwa vibaya kwenye goti la Ronaldo na mchezaji huyo kupepesuka kidogo na kisha kuendelea kucheza kana kwamba hakuna jambo lolote lililotokea.
"Kama bondia angelipata konde kama hilo kichwani, angechukuliwa nje ya ulingo haraka" anasema daktari huyo. "Mabondia wanapoonyesha dalili za kupigwa vibaya ulingoni, hupewa muda maalumu wa kupumzika wa wiki nane, wakati wote ukichunguzwa kama damu zitavuja kwenye ubongo au la", anaongeza.
" Kama kutakuwepo kuvuja kiasi kidogo cha damu katika ubongo, dalili pengine haziwezi kuonekana waziwazi. Lakini wakati mwingine damu inaweza kusababisha maumivu makali kutokana na shinikizo la damu iliyovuja kwenye tishu za ubongo na hivyo kutishia maisha ya mhusika.
Wataalamu wa mambo ya ubongo wanasema kuwa, ikiwa mtu amejigonga kwenye nguzo ya taa za umeme, na kisha akawaambia madaktari kuwa hakumbuki vizuri mambo kadhaa, mtu huyo haraka sana atapelekwa hospitali ya rufaa kwa majaribio zaidi.
Lakini sivyo ilivyo kwa wacheza mpira, wao uamuzi uko kwao kama wataingia tena uwanjani kuendelea kucheza au la!.
Wachezaji 53 wa ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi walifanyiwa uchunguzi na kati yao, 45 walithibitika kuwa na dalili za majeraha ya kutisha kwenye ubongo wao; majaribio kama hayo mara nyingi hufanyiwa mabondia na hushauriwa kustaafu mchezo huo kufuatia matokeo ya uchunguzi huo.
Bondia Frank Bruno alilazimika kuacha ngumi baada ya kupata matatizo ulingoni
Unaweza kupata web sity zenye mambo malimbali hapo chini
www.whisper.2.u.com
www.bbc.co.uk
Unaweza kusaidiwa namna ya kupambana na matatizo ya kupata rafiki
www.televar.com
Kila siku napokea e mail nyingi toka kwa watu mbali wakitaka ushauri
www.infoseek.com
Mbinu mbali mbali utafundisha namna ya kukabiliana na matatizo ya kiafya
www.blackstar.co.uk
www.nbc.com/passions/ Unatakiwa uwe mwanamichezo wa mchezo wowote
www.cnn.com
Kila mtu anatikiwa kuwa makinina kazi yake hivyo umakini ni muhimu sana kwa mchezaji
www.reuters.com
Wanakaribishwa watu wasiokuwa wanamichezo kuuliza maswali
www.zanzibar.or/ziff
Be sure to place a description of your link for your viewers here!
www.emeagwali.com
Unaweza kupata marafiki wa karamu kama utaponyeza sehemu hiyo ya palnet kama unataka!
www.penpalnet
unaweza kupata tamthilia ya passion pamoja na historia za waigizaji wa tamthilia hiyo!
|