Free Web Hosting Provider - Web Hosting - E-commerce - High Speed Internet - Free Web Page
Search the Web

Home | Mimi ni Nani | Movie  | Malimwengu | Contact | Michezo | Ngumi | Muziki | Mila | Mavazi | Makala | Guest Book | penpals | Tabia za wasanii | Visa vya wasanii | Maisha ya wasanii | Marafiki | Makala | Realblog | Photoalbum
KARIBU DILUNGA PAGE

Pata undani wa wangu hapa


Wellcome to dilungahaji Home page.This site is only very basic as my knowledge of HTML.As my knowledge grows, hopefully so the comparative quality of my site will grow.
Unfotunately due full time work,time is a precious commodity for myself and I don't know how regular I will be able to update the site.

Each individual section of the site should give an idea of how often it will be updated.For those who speak Swahili language should check in for some news,penpals,feature, which will be update as the time allow!for my picture and background just see on homepage.

Hope you enjoy the site and if you have any comments then feel free to email me using Contant Me link.


PATA UNDANI WANGU KUHUSU MIMI

Naitwa Haji Dilunga ni mwandishi wa habari,ninayependa kuandika habari za burudani, utamaduni, sanaa, muziki, michezo, mila na jadi.

Kwa vile na penda kudadaisi vitu na kufanya uchunguzi,nimefanikiwa kugundua mambo mbali mbali ya maisha na tabia za watu.

Habari na makala zangu nilizoandika zilionekana na kusomeka katika magazeti mbali mbali ya Tanzania kama magazeti ya Motomoto,Tanganyika Leo,Bahari,Baraza,Democrat, Majira na Dar Leo kwa nyakati tofauti.

Mbali ya kuwa mwandishi, .

Ujumbe muhimu

Usichopenda wewe usimfanyie mwenzako,
Cheo ni dhamana mtu yoyote anaweza kukipata,
Ukijiona wewe bora kuliko wenzako lazima utachukiwa.Kila unapofanya ubaya unatakiwa kujiuliza mambo ninayofanya kama nikifanyiwa mimi naweza kukubali.

Kabla ya kufanya jambo lolote baya jaribu kufikilia kama ungefanyiwa wewe ungeweza kuvumilia, kama utapata jibu la kwamba huwezi kuvumila basi sio vizuri kumfanyia mwenzako.

Unatakiwa kufahamu kuwa duniani ni sehemu ya kupita, kuna sehemu ambayo binadamu wote tutakutana na kuanza kupokea hukumu ya matendo yetu,kama kweli wewe unaamini kama kesho kuna moto ambao watachomwa wale wenyewe tabia mbaya kwanini usibadilike na kuwa mtu mwenye tabia nzuri.

Si kulazimishi kufanya kama nivyoshauri ila ni vizuri ukifahamu kuwa ipo siku ubaya unaofanya kwa wenzako utakuja kukurudia na kujiona kama mtu mwenye mkosi.

Ushauri muhimu

Kuwa makini na wale wote wanaopenda kujikomba kwa mtu mwenye uwezo wa fedha au cheo, kama nyingi watu wanaopenda kujikomba wanakuwa na tabia ya kujidhalilisha na hata kuwadhalilisha wenzao ili mradi mambo yao yafanikiwe.

Watu wanaojikomba wako teyari kutoa hata dada zao ama ndugu zao kwa ajili ya kumfurahisha yule anayemhisi ndio msimamo wa maisha yake.

Wanaopenda kujikomba wanahatari ya kugeuzwa mashoga kama yule anayemuona ni mjanja kwake akitaka kumfanyia vitendo vya kihuni.

Penye udhaifu majungu uchukua nafasi yake.Usipende kulalamika kila wakati watu watakudharau na kukuchoka.

Unapokuwa na shida si vizuri kumweleza kila mtu kunawengeni wanaweza kufurahiya namna unavyoangaika na shida yako.



Taratibu za maisha

Usiwe na marafiki wengi, pia usiwe na maadui wengi, unatakiwa kuwa karibu na kila mtu bila ya kujali kama maskini ama tajiri.Unatakiwa kufahamu umuhimu wako katika jamii na nafasi yako kwenye serikali yako.

hdilunga@hotmail.com

Kila kitu kinawezekana
Katika maisha hakuna kitu kisiwezekana, kila kitu kinawezekana kufanyika, kinachotakiwa ni kujituma na kujali kile unachofanya katika kunyanyua maisha yako na kuboresha.


Ubabaike kuona mtu fulani anakusema vibaya, inawezekana anakusema vibaya katika mazingira ya kutaka kukatisha tamaa ili isifanikewe katika maisha.


Watalaam wa saikolojia wanasema mtu aliyekata tamaa ya maisha anapenda sana kutumia muda wake mwingi kuwakatisha tamaa wenzake wanaotafuta maisha, kwa hiyo kauli za watu kama hao sio vizuri kuzisikiliza.


Ukimuona mtu anapenda sana fedha lazima ufahamu kuwa ni khatari kwa sababu naweza kufanywa chochote ama kufanya chochote kwa ajili ya kutaka fedha.




Kwa wale wanaopenda kubadilishana mawazo na kujadiliana mambo mbali mbali ya maisha kama mapenzi, burudani, siasa, uchumi, jamii, na mambo yote yanayohusu jamii ya kitanzania.

Katika kujadiliana hakutakiwi mtu kutumia lugha ya matusi, Ingawa itakuwa vigumu kuanza kuchunguza baadhi ya mambo yatakayoandikwa lakini tunaamini watakajadiliana watatumia lugha ya nzuri.

http://www.pollhost.com/admin.cgi


Ukitaka kupanda uhundo endelea kusoma page kwa makini