Pata maelezo ya Sinema kwa ufupi
Sinema ya Uwanja wa Dhambi
Sinema inaanza kwa kumuonyesha Mwanamke anayeitwa Mama Shubiri akipanganga vitu vyake vya kichawi katika mkeka. Kamera vitu ni vyungu vitatu, usinga, vibuyu, dawa za unga, mayai yaliyoandikwa, glass, chupa zenye marashi, ungo ulijaa mjani, vitamba vyekundu vimetandikwa, kisu chenye ncha kali. Pia inaonyesha moto unaowaka. Nje barabarani kwa mbali waonekana wenzake wakiwa wamevaa mavazi mekundu na meusi, wakitokea makaburini huku wakiwa wamebeba maiti ya mwili wa Mwanaume.(ambaye ni Mzee Joshua) Wanaonekana wakitembea huku wakiimba wimbo wa kichawi. (Tumemwita amekuja, mwana wa binadamu.Eeee amekuja. Mwana wa bindamu.Chakula chetu nyama. Kinywaji chetu damu.) Mama Shubiri anasikia sauti ya wenzake. Ananyanyuka na kuanza kucheza huku akiimba. Wanaonekana wamefika na kuiweka maiti juu ya mkeka karibu na chungu kikubwa. Mama Shubiri anamchoma na kisu tumboni na kuanza kunywa damu. Wenzake nao wanakunywa damu hiyo. Kutokana na kupenda kufanya vitendo vya kichawi, anamua kumfanya mumewe kuwa ndondocha na kumtumisha kama mfanyakazi wake wa ndani. Anamgeuza mumewe kama kistuli cha kuwekea miguu. Anamsaidia binti yake Shubiri kuchukua mwanaume wa msichana anayeitwa Jamila. Wakati binti huyo anapokuja kumtaka mtoto wa Mama Shubiri kumwachia mume wake. Mama Shubiri anaamua kumfanya ndondocha kwa ajili ya kumkomoa binti huyo na mumewe anachukuliwa na mtoto wake Shubiri. Kama haitoshi Mama Shubiri anataka kumuua mtoto wake wa kufikia.Anashindwa kufanya hivyo kutokana na nguvu za ajabu alizopewa na Malaika. Ikimbukwe kuwa majirani zake wengi amewaingilia kiuchawi nyakati za usiku na kuwafanyia vitendo vya kichawi. Amemuingilia mpaka Mganga wa kienyeji na kumchukua kumfanya ndondocha. Hayo ni baadhi ya matukio yaliyokuwa katika sinema hiyo ya uwanja wa dhambi. Ni dhambi kweli zilizofanyika katika sinema hiyo.
Sinema ya Picnic
Sinema hiyo inaonyesha maisha ya vijana wanavyodanganyana na kuingia katika matatizo makubwa.Ni sinema inayosikitisha na wakati mwingine kukufanya uwachukie waigizaji kutokana na vitendo vyao wanavyomfanyia Dora.Mtunzi alikuwa makini katika kutunga sinema hiyo iliyokusanya visa vinavyovutia kuangalia na mpangilio wa maneno usichosha kusikiliza.Wasanii wamecheza kwa kiwango cha hali ya juu, kila msanii ameweza kushika husika wake. Kwa ufupi sinema inaanza kwa kuwaonyesha Vijana wanaokwenda Picnic Bagamoyo kutembelea Magofu ya Kaole.Wakiwa katika magofu ya Kaole, mzimu wa Dora unawatokea na kuanza kulipa kisasi kwa kuua kila aliyekwenda huko. Hebu pata picha ya magofu yanavyotisha alafu unatokewa na mzimu. Kwa kweli inasikitisha na kuogopesha.Picnic ya furaha imegeuka kuwa ya majonzi. Mtazamaji akianza kuangalia hata kubali kunyanyuka mpaka hakikishe imekwisha. Ni sinema ambayo kila aliyehusika alijituma kuifanya iwe nzuri na kuvutia, kuanzia kwa mpigaji picha Matheas Charange, alipiga picha nzuri za kuvutia tofauti na wapigaji picha wengine ambao picha zinaonekana kama zinafifia.Muongozaji wa sinema hiyo ambaye ndiye mtunzi Haji Dilunga ameongoza katika kiwango cha hali ya juu. Amehakikisha kila msanii ameweza kuvaa husika wa nafasi anayocheza.Mhariri wa sinema hiyo Ngema Andrew alionyesha uwezo katika kuhariri. Hasa katika vile vipande vinavyomuonyesha Mzimu wa Dora anavyotokea ghafla na kuyayuka.Unaweza kujiuliza ni wasanii gani waliocheza sinema hiyo. Ni Mwajuma Abdul a.k.a Maimuna kama Dora,Aisha Chanzi a.k.a Mama Shubiri amecheza kama Mama Dora, Fatuma Hamisi amecheza kama Salome Wengine ni Fidelis Njoka kama Juto, Rahma Njau kama Naomi, Johari Ramadhani kama Salama, Noela Boniface kama Neema. Danny Komba kama Mganga, Omari Mtomea kama Jimmy, Obbi Lubindo kama Ben. Sinema hiyo inatarajia kuingia sokoni wakati wowote kuanzia sasa.