Free Web Hosting Provider - Web Hosting - E-commerce - High Speed Internet - Free Web Page
Search the Web

Home | Mimi ni Nani | Movie  | Malimwengu | Contact | Michezo | Ngumi | Muziki | Mila | Mavazi | Makala | Guest Book | penpals | Tabia za wasanii | Visa vya wasanii | Maisha ya wasanii | Marafiki | Makala | Realblog | Photoalbum
Ukweli Kuhusu Maisha na imani ya ukimwi

Siku ya wapendanao ni kuambukizana ukimwi
SIKUKUU ya valentine day maarufu hapa Tanzania kama siku ya wapendanao imekuwa ikipokewa kwa nadharia tofauti na inavyotakiwa kwa wale wanaosheherekea .Baadhi ya watu wanajikuta wakiunganisha siku hiyo na mambo ya ngono na matokeo yake kupata maambukizo ya ukimwi.

Nadharia hiyo iliyojengeka miongoni mwa Watanzania, imesababisha watu kuamini ni siku ya kuonyesha upendo wakweli na dhati kwa mahawara, vimada, nyumba ndogo na sio kwa wale wapenzi wao wa kweli ambao ni wake zao au waume zao.

Kwa wale wasiolewa na kuoa , katika sikukuu hiyo wamekuwa wakionyesha upendo kwa wapenzi wao wapya badala ya wapenzi wao wa zamani, huku wakisahau kwamba siku hiyo inakuwa ni siku ya kujipatia virus vya ukimwi.

Wengi wanachukulia siku hiyo kama siku ya kwenda kupumzika na wale wanaohisi ndio wanawapenda badala ya kupumzika na kuonyeshana upendo wa kweli, na wake zao ama waume zao.

Uchunguzi uliofanyika katika siku za wapendano zilizopita, umegundua kwamba wanaume wengi wanakwenda katika kumbi za burudani kustarehe na vimada badala ya wake zao, sambamba na wanawake wanavinjari na waume za watu, Katika hilo la kuchukua mahawara, wanaongoza katika kuonyesha upendo na kuchukua mahawara ni wanaume.

Kwa wale watu ambao wake zao wanajulikana walionekana na wanawake wengine , huku wakionyesha wasi wasi wa kuonekana na watu wanaowafahamu ambao wanaweza kwenda kuwaeleza wake zao.

Katika hali kama hiyo hakuna maana ya kusheherekea, kwa sababu pale panafanyika ngono na hatari kwa maisha yao kutokana na kuwepo kwa gonjwa la ukimwi. Wanaojijali wanatoka na wapenzi wao wa kweli badala ya kujitumbukiza katika sakata la kutoka na vimada ambavyo baada ya muda vinasababisha ugomvi wa kugombewa na wanaume wengine wanaojidai kuwa wanawamiliki wanamke hao.Hata hivyo vimada wanaweza kumsababishia mtu ugomnjwa wa ukimwi.

Siku ya wapendao ni siku ya kuonyeshana upendo wa kweli kwa wale wanaopenda, sio lazima awe mke ama mume, inawezekana kuonyesha upendo kwa dada, kaka, baba, mama, babu, bibi , shangazi , mjomba, rafiki na kadhalika.

Ndio maana siku hiyo ikaitwa siku ya wapendanao na sio siku ya wapenzi, ingekuwa siku ya wapenzi hapo kweli unatakiwa kuonyesha mapenzi kwa yule unayetaka kuwa naye karibu na kufanya naye ngono.

Kwa sababu ni siku ya wapendano ndio maana watu wamejipangia kuwa ni siku ya kuonyeshana upendo kwa wale wanaopendana, kwa hiyo ndio maaana wanajikuta wakiwapenda wapenzi wao hasa wale wa nje ya ndoa badala ya wake na waume zao.

Kwa wale walioa au kuolewa wanatakiwa kuonyesha upendo siku hiyo ya tarehe 14, siku hiyo ikipitiliza hakuna maana ya kutoa zawadi kwa yule unayempenda,Zawadi inakuwa na umuhimu katika siku inayohusika.

Mwanaume anatakiwa kuonyesha upendo kwa mkewe kwa kumnunulia zawadi kama vile kadi,maua, sambamba na zawadi nyingine, kama unawezakufahamu saizi ya chupi anayovaa unatakiwa kumnunulia chupi.

Si vibaya kwa wanamke kumkumbusha mumewe kwa kumwandikia kiujumbe chenye maneno machache na kumwekea katika shati lake bila mwenyewe kujifahamu ili akiingiza mkono mfukoni aweze kushangaa.

Unaweza kumwandikia mpenzi wako kuwa siku ya wapendanao imewadia naomba unikumbuke mpenzi wako fulani.Baada ya kufanya hivyo naye anaweza kukumbuka kwa kukutafutia zawadi hiyo.

Siku hiyo iliwekwa na watu fulani kwa ajili ya kumbukumbu ya mtu mmoja kwa jina la Mtakatifu Valentino, ambaye aliuawa kwa kukiuka matakwa ya watawala wa wakati wake, kwa sababu alikemea baadhi ya mila zao na akawa anafungisha ndoa zilizopigwa marufuku katika wakati huo.

Pengine walioiweka siku hii walikuwa na maana nzuri kabisa. Tatizo ni kwamba siku hizi zimepewa tafsiri na matumizi tofauti na baadhi ya watu ambao wanapenda ngono. Watu wengi huzipa sifa siku hiyo kwa matumizi kwa jinsi wanavyopenda wao.

Baadhi ya watu wanafahamu kuwa siku ya wapendanao ni kwenda beach kupunga upepo kama Wazungu, au kwenda kwenye majumba yanayoitwa ya starehe na vimada au mahawara..

Ukichunguza kwa makini utakuta kwamba siku ya Valentino imekuwa ni kinyume tu cha Siku ya Ukimwi Duniani. Katika Siku ya Ukimwi Duniani, watu hutafakari jinsi ya kupambana na gonjwa baya la zinaa lililokumba dunia. Redio na magazeti ya maana duniani hushiriki katika kuhamasisha mapambano dhidi ya ukimwi.

Kinyume chake, Valentine Day imekuwa ni siku ya kuwashawishi watu siku hiyo "wapendane zaidi hasa kwa wasiokuwa wanandoa". Basi kila mtu siku hiyo atahakikisha haipiti bila ya "kupenda".Baadhi ya redio siku hiyo ndiyo itapata fursa ya kuhamasisha watu. na kuwatangazia mambo, yasiyofaidisha jamii kwa lolote.

Utakuta watangazaji wa vipindi vya redio za jijini yaani FM stereo siku watatangaza na kuwashawishi watu kuwa wawili wawili huku wakijua kwamba wengine ni wanafunzi wasiotakiwa kujishughuli na mambo ya mapenzi.

Kama suala ni kupenda, basi kwa watu wengine kila siku kwao ni Valentine Day ni siku ya wapendanao,kila siku kwao ni Valentine, kwa sababu hawangojei siku ya kupangiwa kumpenda wanaowapenda, yaani wake wao. Wale wanaosubili kupangiwa ni wale wanaopenda kuwa na vimada na mahawara..


WANAOJIJALI WANAKUBALI KUWA NA MPENZI MMOJA

KWA wale watu wanaojijali wanakubali kwamba kuwa na idadi ya wanawake au wanaume ni kujishushia heshima mbele ya watu wanaojali ubora wa afya yao na kuwa makini na maendeleo ya maisha yao na kizazi chao.

Wengi wanaojifanya ni vifaru wa kutafuta wasichana au wanaume wanasumbu na matatizo ya akili yanayotokana na kutojifahamu, wao ni nani katika jamii, wamekuja duniani kufanya kitu gani.

Watu wengi wenye tabia hiyo wanadhani kama wamekuja duniani kutafuta mali, umaarufu, kunywa pombe, kuiba na kunyanyasa wenzao katika hali yoyote.

Lakini wanashindwa kufahamu kuwa baada ya kupata hivyo vyote ni wanachopata,Utakuta hakuna wanachopata zaidi ya kuendelea kufanya mambo hayo yasiyokuwa na maana na hatimaye kufa huku wakiwa bado wanapenda kuwepo duniani.

Kitu cha dakika 3 kinaweza kukuweka kitandani kwa muda wa miaka miwili na hatimaye kufa.

Inakuwaje kitu cha dakika 3 kikupoteze muda wako na hatimaye kuwa katika matatizo yatakayopelekea kuwa katika ulimwengu wa kifo.

Katika maishayangu yote sijawahi kuona kaburi la mtu aliyekufa kutokana na kushindwa kustamili tamaa ya mwili wake,ila nimeweza kuona makaburi ya watu waliokufa kwa sababu ya kuendekeza tamaa ya miili yako.Yaani kupenda kufanya zinaa na hatimaye kupata gonjwa la ukimwi.












Pata taarifa mbali mbali kupitia page hii