Free Web Hosting Provider - Web Hosting - E-commerce - High Speed Internet - Free Web Page
Search the Web

Home | Mimi ni Nani | Movie  | Malimwengu | Contact | Michezo | Ngumi | Muziki | Mila | Mavazi | Makala | Guest Book | penpals | Tabia za wasanii | Visa vya wasanii | Maisha ya wasanii | Marafiki | Makala | Realblog | Photoalbum
MALIMWENGU

Kisima chenye maji yachemkayo Rufiji


Wilaya ya Rufiji iliyokuwa mkoa wa Pwani ina kisima cha ajabu ambacho watu wengi hasa waganga wanakitumia kutatulia matatizo ya wateja zao.

Mmoja wa wakazi wa wilaya hiyo alijitambulisha kwa jina la Mzee Maulid Uvuruge alisema maji hiyo yanasaidia kutibu magonjwa ya upele, matumbo, nuksi,mikosi, kutopata mimba, nguvu za kiume, kupata bahati ya kazi ama katika biashara.

Alisema anayetaka kufika katika kisima hicho anapelekwe na watu wanaofahamu njia ya kwenda huko,kwa sababu kuna sehemu ambazo kama ukikanyaga unaweza kuzama katika tope na kuwa ndio mwisho wako.

Uvuruge alisema hata wachungaji wanaogopa kupitisha ng'ombe zao karibu na eneo hilo kwa kuogopa kuzama katika tope,

Uvuruge alisema kisima hicho kipo katika eneo la Utete Bomani. Mji huu ndio makao ya wilaya ya Rufiji.

Uvuruge alisema mji huo una sehemu moja ina maajabu makubwa sana. Ni juu ya mlima ambao ni mrefu kiasi. Mambo yaliyopo katika mlima huo ni ya maajabu sana kama mtu ataangalia kwa macho.

Alisema juu ya mlima huo kuna kitu kama tundu ambalo ni refu sana kwenda chini. Ni sawa na kisima kwa urefu.Unapochungulia tundu hilo utakachokutana nacho ni maji mengi yaliyojitokeza mpaka kwenye mdomo wa tundu hilo.

Uvuruge alisema cha ajabu ni kwamba maji yanaonekana kama vile yanachemka na utaamini hivyo kwa sababu maji hayo ni moto sana, tena yanatoa mvuke. Wenyeji wa hapo wanasema hata ukitumbukiza kitu kama boga linaiva.

Alisema kutokana na maajabu hayo imekuwa ni jambo la kawaida kwa wasafiri kusimama hapo kununua kutoka kwa wenyeji vitu kama maboga na mihogo na kisha kuifunga kwenye majani au mifuko ya nailoni na kuitumbukiza kisimani humo kwa kutumia kamba ndefu kama vile wanachota maji.

Baada ya dakika kama kumi mtu hushikilia kamba hiyo na kisha kuivuta. Ndipo unapokuja kushangaa kuona kwamba kile kilichotumbukizwa kimeiva kama vile kimepikwa jikoni.

Dakika 10 tayari kilichotumbukizwa katika kisima hicho kimeiva na teyari kwa kuliwa. Watu wakila wakimaliza wanafanya safari ya kwenda Kilwa au Dar es Salaam, wakati huo kulikuwa na usafiri wa kubahatisha sio kama hivi sasa kuna usafiri wa uhakika.

Maajabu ya sehemu hiyo hayaishi hapo. Chini ya kisima hicho kuna sehemu inatoa maji hayo yanayokwenda kwenye mto. Kabla ya kufika uko mtoni yanapita katika jiwe au tuseme jabali moja lililotandika kama mkeka.

Alisema maji hayo ya moto yakifika katika jabali hilo yanabadilika kama sio kupoa, watu kuweza kuoga kwani yanakuwa yamepoa na hayachemki tena kama yanapokuwa ndani ya kisima kile.

Watu wanaotoka Bomani asubuhi huenda kwenye jiwe hilo kuoga maana hawawezi kwenda kule kwenye kisima kutokana na ukweli kwamba maji yake ni ya moto sana.

Uvuruge alisema mambo hayo yametokea zamani na mpaka sasa bado kisima hicho kipo."Ni mambo ya zamani ya karne kwa karne. Sijuwi kwa nini viongozi wa wilaya wanashindwa kuitangaza sehemu hii kwa ajili ya utalii. Hii ni sehemu ambayo ina kivutio cha aina yake ambacho kinaweza kumfanya mtalii yeyote kuwa tayari kulipa gharama yoyote ile ili mradi ayaone maajabu haya",alilalamika Mzee Uvuruge.

Alisema kitu cha ajabu kuhusu haya maji ni kwamba hayapoi kabisa,.alisema hata mvua iwe mzito kiasi gani . Na wala hayazidi moto hata lipige jua kali kiasi gani.

Uvuruge alisema maajabu hayaishii hapo. Sehemu hiyo ina miti mikubwa inayochangia katika kuongezeka maji na ule uvuguvugu uliopo hapo.

Miti hiyo inafanya sehemu hiyo kuwa na vivuli vingi vizuri ambavyo hufanya mandhari ya sehemu hiyo kuwa mwanana kabisa kwa watu wanaotembelea hapo.

Lakini pamoja uzuri wa sehemu hiyo, pia kuna hatari zake ambazo unaweza kusababisha mtu kupoteza maisha.

Hatari hiyo ni kwamba baadhi ya sehemu za eneo hilo kuna ardhi yenye tope zito. Ni kwamba mtu ukitumbukia tu kwenye tope hilo unaweza kupotea na usionekane tena.

Ni sehemu ambayo inahitaji tahadhari sana na uzoefu wa hali ya juu ukifika katika eneo hilo.Kuna tope zito sana na wala halikauki wala kulainika ...lipo hivyo miaka nenda rudi.

Alisema eneo hilo kwa kweli lina hazina kubwa kwa maendeleo ya mkoa wa Pwani na taifa kwa jumla. Ubaya zaidi ni kwamba eneo hili lipo katika njia ambayo watalii wanaitumia kwenda kuangalia wanyama huko Mbuyuni, Mtemele na Kingupila.

"Si nia yangu kujaribu kuwafundisha watu kazi zao, lakini kwa kweli mimi najisikia uchungu sana ninapoona viongozi husika hawachukui tahadhari yoyote ile ili kuliendeleza eneo hilo kwa ajili ya kuvutia watalii. Kwa kuendeleza kama lilivyo bila kuendeleza, naamini wilaya, mkoa na hata taifa hupoteza mamilioni ya fedha kwa njia ya utalii.


Unajua ni kwa nini pakaitwa Magomeni Mapipa?

KATIKA mji wa Dar es Salaam hapo zamani hakuna sehemu iliyokuwa inaitwa Magomeni Mapipa. Hili jina lilijitokeza maea tu ilipojengwa barabara ya Morogoro Road kama inavyojulikana kwa Kimombo.

Hii barabara ilianza kutengenezwa mwaka 1951 na kumalizika mwaka 1954. Katika kipindi hicho ndio likapatikana jina la Mapipa.

Upande mmoja wa barabara ya Morogoro ukaitwa Mapipa na ule mwingine ukaitwa Makuti, katikati ndio ujenzi wa barabara hiyo, upande mmoja uliitwa Mwinyimkuu Mshindo.

Sasa ikawaje upande huu mwingine ukaitwa Mapipa? Naamini watu wengi hawajui. Bila shaka wengi wanafahamu kuwa sehemu inapotengenezwa barabara ya lami hapakosi lami, na penye lami hapakosi Mapipa.

Basi watu wa upande ule ambao hadi leo unaitwa Mapipa wakaanza kuyachangamkia yale Mapipa ya lami. Wakayazoa kwa wingi ili waweze kuezeka nyumba zao. Nyumba nyingi za upande ule zikajikuta zimeeezekwa kwa Mapipa. Ule upande mwingine watu wake wakabaki na yale makuti yao.

Nyumba nyingi za upande ule zikaendelea kuwa za makuti na upande huo ukaendelea kuitwa Magomeni Makuti na ule upande wa viezeko vya Mapipa ukajipatia umaarufu wa jina la Magomeni Mapipa.

Isitoshe kule bondeni nako yalichimbiwa mapipa mpaka kule juu ili kuzidisha uimara wa barabara.

Pale darajani napo yakawekwa mapipa mengi tu kwa lengo la kulifanya daraja hilo kuwa imara kwa magari hata yale makubwa ya mizigo.

Hapo ndipo pakakamilika barabara ikawa hivi sasa. Likaanza jina la Magomeni Mapipa nalo likatawala sana. Ule upande mwingine ukabaki kuitwa Makuti, kwa sababu tu kwamba upande huo uliendelea kuwa na nyumba zilizoezekwa kwa makuti.

Kama nilivyosema awali, kabla ya kujengwa kwa barabara ya Morogoro hapakuwa na jina la Mapipa. Chanzo cha kuitwa jina hili ni hii barabara ya Morogoro ambayo ujenzi wake uliambatana na mlundikano mkubwa wa mapipa ya lami yaliyosambaa kuanzia kule inakoanzia barabara ya Bagamoyo mpaka pale darajani hadi Magomeni penyewe.

Sasa labda niongezee suala lingine kidogo katika hii hii barabara ya Morogoro. Pale zinapoanza barabara, za Morogoro na Bagamoyo zamani paliitwa Mwembe Togwa.

Pale ndipo safari za kwenda Bagamoyo zilipokuwa zinaanza. Lazima ufike pale ndipo uulize magari ya Bagamoyo kama yashafika au bado, jibu utapata pale maana kulikuwa na mtu maalumu kazi zake zilikuwa ni kupanga safari za aliyekuwa anajua magari yako mangapi na lipi litaanza kuondok. Mabasi yalikuwa yanaondoka kwa utaratibu huo, kuanzia la kwanza hadi la mwisho. Na kwa kawaida yalikuweko mabasi manne tu.

Tukurudi tena kuhusu masuala ya barabara ya Morogoro, utakuta kwamba kabla ya kujengwa hii ya sasa, iliyokuwa inaitwa barabara ya Morogoro ni ile ambayo iliwahi kuitwa Pugu Road ambayo sasa inaitwa Nyerere Road.

Ile ndiyo ilikuwa barabara ya Morogoro. Ulikuwa unakwenda na ile mpaka Kisarawe kuelekea Morogoro. Ilikuwa ni kazi ngumu kusafiri kwa njia ile kwenda Morogoro. Watu walikuwa wanakubali kusafiri kwa treni kuliko mabasi kutokana na ugumu wa safari ya basi.

Ukitoka Kisarawe unafika Kazimzumbwi, Ruvu Kivukoni, Ngerengere, Mikese hadi Morogoro. Hiyo ndio ilikuwa safari ya kwenda Iringa na kwingineko.

Usumbufu ulikuwa pale Kivukoni Ruvu. Pale watu walikuwa wanalala hata siku mbili pantoni ikiharibika kutokana na matatizo mbalimbali kama vile kupitisha magari makubwa yenye mizigo mizito. Kutokana na sababu hiyo, ilikuwa ni kama miujiza mtu kuondoka Morogoro na kufika Dar es Salaam siku hiyo hiyo. Ilikuwa ni safari ndefu sana na iliyojaa usumbufu mkubwa. Safari kati ya Morogoro na Dar es Salaam, ambayo leo hii ni suala la saa kati ya mbili na tatu, zamani ilikuwa ni msafara wa kati ya siku mbili au tatu!!!.




Kisa cha kunyongwa Kibasila

KWANZA Kibasila mwenyewe siyo aliyongwa, aliyeyongwa ni mtoto wake Kibasila. Huyu mtoto aliitwa Digalu Kibasila. Digalu alikuwa mtoto wa nne wa kibasila.

Wa kwanza aliitwa Geruka, wa pili Bugugusu, wa tatu Salehe, wa nne ni huyo Digalu bin Kibasila. Huyu aliwahi kuwa kiongozi wa vita vya Majimaji.

Digalu alikuwa mmojawapo wa watu waliochukia kutawaliwa na Wazungu,enzi hizo wakoloni wa Kijerumani.

Ndiyo maana Wajerumani walikasirika sana walipogundua kwamba Digalu alikuwa miongoni mwa washiriki wa vita vya Majimaji. Wakaazimia kufanya utafiti wa hali ya juu kuhusiana na taarifa hizo.

Siku moja likatokea tukio la kuuawa kwa liwali mmoja katika sehemu iliyoitwa Machinga kule Msanga.

Hii ni sehemu yenye, kilima kabla ya kufika kijijini Msanga penyewe. Tena huyu liwali aliuawa kwa kuchomwa mshale.

Upelelezi mkali ukafanywa kujua nani aliyehusika na mauaji ya liwali yule. Ikabainika kwamba liwali yule alikuwa ameuawa na wapiganaji wa Majimaji, tena wakiongozwa na Digalu Kibasila.

Liwali huyo alikuwa akiishi Masaki. Alikuwa ametoka Masaki siku hiyo kwenda bomani Kisangile kikazi. Alipofika hapo kilimani akakutana na jeshi la Majimaji. Liwali huyo alikuwa amepanda farasi.

Wale wanajeshi wa Majimaji wakamuua mtumishi huyo serikali ya Kijerumani kikatili. Farasi akapona na akafanikiwa kwenda peke yake mpaka Msanga kijijini.

Ukawa ni mshangao mkubwa kwamba farasi kafika peke yake bila mtu. Ndipo watu walipotoka pale Msanga kufuatilia kulikoni. Walipofika pale kilimani wakakutana na maiti imelala barabarani. Kumbe ile maiti ilikuwa ya liwali.

Hawakujiuliza maswali mengi. Wakajua ni lazima tu kazi ile ilikuwa imefanywa na askari wa Majimaji.

Hazikupita siku mbili ukweli ukabainika kwamba askari wale wa Majimaji ndio waliohusika na mauaji yale, wakiongozwa na yule yule Digalu Kibasila.

Watawala wa Kijerumani wakaandaa sehemu fulani hapa Dar inayoitwa leo hii Kibasila kwa ajili ya kumnyonga huyo Digalu. Wilaya zote za mkoa wa Pwani - Kisarawe, Mafia, Rufiji na Bagamoyo- zikapewa taarifa kuhus shughuli ya kunyongwa kwa Digalu. Watu wakatakiwa kufika wajionee jinsi Digalu atakavyonyongwa mbele ya kadamnasi.

Wakoloni wa Kijerumani walitelekeza ahadi hii ya mauaji ya Digalu.

Ilikuwa ni siku ya Ijumaa, saa tano asubuhi, mpiganaji wa Majimaji aliyechukua utawala wa Kijerumani, Digalu bin Kibasila alinyongwa. Sehemu aliponyongewa ni pale ambapo panaitwa Mwembe Kibasila. Na hii ndio sababu sehemu ile inaitwa Mwembe Kibasila.


Hasara ya Wilaya ya Kisarawe kukosa pesa

NASIKITISHWA na wilaya ya Kisarawe kwa kutoitumia hazina yake nazungumzia ile nyota iliyoko kule Chang'ombe tarafa ya Mwanarumango kupotea bure msituni bila ya faida nasema hivyo kwa uchungu nimeona kwa jicho lango mkoa wa Mbeya wilaya ya Mbozi njia ya kwenda Tunduma hapo hapo boani kuna nyota imeanguka zamani kuliko hii ndogo ukilinganisha na hii yetu lakini imehifadhiwa na kujengewa kijumba kizuri na kukazungushwa ukuta ili mradi ukifika utapenda.

Kukawekwa wahudumu wawili kukaribisha wateja kwa malipo maalum kwa pesa yoyote ile ya hapa au ya kigeni wanapokwenda kuona nyota wilaya inapata fedha nyingi sana.

Watu kutoka Zambia kwenda Mbeya wanasiommama wakiona lile bao linasema pita uone nyota ya ajabu mara nyingi huja hata watalii kutoka Malawi au Zambia.

Je, Kama na viongozi wa Kisarawe ningefanya hivyo nisingepata vijipesa japo kidogo ili wilaya ipate japo kidogo.

Kuna mengi ya faida katika wilaya ya Kisarawe mbali na nyota ya Chang'ombe kuna mengine nayo japo kutoka KIsarawe kuelekea Chang;ombe kuna kijiji kinaitwa Kibutu tarafa ya Sungwi hapo kwa upande wa kushoto ukitoka Kisarawe kuna mlima mkubwa na msitu mzito sana.

Mlima huo unaitwa Mwanamzungwi mlima huu haupandiki kwenda kileleni sababu zake nyingi kwanza kuna kiza kizito pili msitu unatisha sana zama za nyuma wazee walikuwa wakilima chini ya mlima, mipunga, mitama na mazao mengine lakini wengi wao walishindwa kuendelea na kilimo hicho kwa sababu za miujiza mingi ya namna ya kwa maana ya usiku na mchana mara unaweza kusikia watu wababwata kama kwamba kuna majumba.

Mara nyingi utasikia kilio kikubwa sauti za wanawake na wanaume sauti mchanganyiko utadhani mahali kuna mji mkubwa na watu sasa wamefiwa mara utasikia ngoma zinapigwa karibu sana na mashamba lingine ukielekea sana bondeni utakuta mchana unameta meta sana ukiweka kizani na uwe kwenye chombo au karatasi utastuka unameta meta sana rangi za namna nyingi tu. Kuna aina ya mawe ya ajabu halafu kuna mmuliko muliko usiku ukitizama mlima.

Kuna wanyama wa namna mbalimbali kuna ndege wa namna mbalimbali na nyingi sana lakini hawatengwi na wakitengwa hawanasi sheti kwa tambiko maalum za maombi hapo unaweza ukapewa au laa usipewe.

Kwa mfano mahali kama hapo hazina ikipatupia jicho hapawezi kutowa faida ya wilaya lakini haya ni mawazo ya kibinadamu sifundishi watu kazi naomba msamaha kwa wote wanaohusika na wilaya ya Kisarawe tutaonana juma lijalo.


Kuna kisima cha kwa Mbena


LEO narudi tena katika wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani kuna mambo mengi hasa yanayohusiana na utamaduni wetu kule Masanganganya.

Kuna kijiji kimoja kinaitwa Kitambo, si mbali sana kutoka pale shuleni ukifuata barabara ya Mwanerumango utafika mahali panaitwa Mibuyu saba.

Ukifika eneo, katika mkono wako wa kushoto utakuwa umeshawasili kitambo.

Hapo ndipo penye hicho kisima kikubwa cha karne kadhaa zilizopita.

Katika eneo hilo pana kichuguu kikubwa sana na pembeni kuna kisima ambacho hakikauki na wala hakiongezeki.

Siku zote kinabakia ni hivyo hivyo.

Kisima hicho kina maji ambayo mara zote ni baridi sana utadhani yamo ndani ya barafu.

Ni maji meupe ambayo hayabadiliki, masafi na hayana chumvi.

Wakati wa kiangazi visima vyote hukauka lakini cha kwa Mbena hapana.

Na wakati wa masika, maji yake hayalingani na ya mvua hata kama yale yanatoka juu ya kile kichuguu hayapiti pale kisimani.

Kitu cha kushangaza ni kimoja, nacho ni kwamba kama maji yale yataonyesha kupungua, watu huanza kuwa na wasiwasi kuwa huenda kuna matatizo na hupeleka habari kwa wale kina Nyegongo ambao ndio wenyewe.

Wale kina Nyegongo hutafuta wakati na siku maalum ambapo huambatana kuelekea huko.

Katika safari hiyo huwa ba michi miwili au mitatu, na yule mzee Nyegongo mwenyewe huenda pale kwa heshima na unyenyekevu mkubwa.

Baada ya kufika katika eneo hilo, hufanya tambiko halafu kama kuna chakula hupikwa. Kuku huchinjwa na kupikwa mchuzi.

Hupigwa ngoma za ile michi na nyimbo kuimbwa. Wale watoto ndio hupiga ile michi katika ile mimbo.

Kuna baadhi ya watu wa zamani na watoto wengine ambao hucheza na huku wanaomba. Wakimaliza kufanya hivyo ndipo hupakuliwa chakula watoto hupewa cha kwao na wakubwa cha kwao.

Wakishakula hurudi majumbani kwao kesho na watu hukuta maji yamejaa sana mpaka yanamwagika.

Pale ndio hujulikana kuwa tambiko yao imekubaliwa na imani hupatikana ya mwaka ule kwani hata wakilima vyakula vitapatikana bila wasiwasi.

Kwa hiyo huzingatia ahadi walizoziweka na ni lazima chochote wanachoahidi wakitimize.

Hata hivyo, mara nyingi huomba vikapatikana na hupatikana kweli. Hii ni kwa sharti mvua inyeshe kwa hiyo tambiko litakuwa limekamilika.

Katika tukio hilo la neema ya mvua watu huwa na furaha kila mahali.

Wakati huo wa furaha watu huamua kucheza ngoma, kusoma hitma, kusoma Maulidi na pia ndio wakati wa kufanya sherehe za harusi mbalimbali.

Huu unakuwa wakati wa amani kubwa kwa vile hakuna watu wanaogombana zaidi ya furaha tu.

Kutokana na amani hiyo, utamaduni wa watu honekana dhahiri kutokana na ngoma mbalimbali pamoja na nyimbo.


Wachina walivyotajirika Dar kwa kilimo cha mboga

HAPO zamani jiji letu la Dar walikuwapo Wachina watatu. Wachina hao ndio kwanza kabisa kuja hapa na kazi yao ilikuwa kulima. Hawa Wachina hawakupenda kazi za kutumwatumwa.

Wao walipofika tu walichofanya ni kutafuta mabonde mazuri yenye rutuba. Wakayapata.

Moja ya mabonde hayo ni kule Ilala katika sehumu iliyoitwa kwa Mohamed Abeid, nyuma ya kiwanda cha bia. Mchina wa kwanza akapata eneo hilo. Naye aliitwa Selemani.

Baada ya muda kidogo na yule wa pili akapata eneo kule Kigogo kwa Selemani Abushiri na watatu akapata kule Keko kwa Bin Akida.

Utajiuliza ni kwa nini yule Mchina wa kwanza aliitwa Selemani. Jibu ni kwamba huyu bwana alikuwa amesilimu.

Huku kusilimu kwake ndiko kulikompatia hilo eneo kwa sababu eneo hilo lilikuwa linamilikiwa na Mwarabu.

Wachina walipopata maeneo haya ya mabonde mara moja wakaanza kulima mboga, mbalimbali kama figiri, kabichi, mchicha, pilipili, nyanya n.k.

Haya ni mazao ambayo watu wa hapa kwetu walikuwa hawajishughulishi nayo sana kilimo chake. Watu wengi walikuwa wanalima mpunga na mazao mengine.

Msimu wa figiri ulipowadia w